OpenIDEO is an open innovation platform. Join our global community to solve big challenges for social good. Sign Up / Login or Learn more

KARIBU KATIKA CHANGAMOTO LA USALAMA WA WANAWAKE

English - Français -   हिंदी  - Español

Jinsi tunaweza kufanya maeneo ya miji yenye mapato ya chini yawe usalama na maisha ya wanawake na wasichana imaarike? 

​MPANGILIO WA CHANGAMOTO


                                           

Wasilisha wazo lako kwa Changamoto la Usalama Wa Wanawake

                                         

 Mawazo bora yatachaguliwa hadi kwenye awamu ya kuboresha. Katika fursa hii, tutawaomba jamii wawasilishe mawazo ziadi ili tupate mafanikio makubwa.

                                         

 Mwisho, Timu ya Kukuza itatangaza orodha fupi ya mawazo marufu na kupeana tuzo hadi dola 500,000 kama msaada wa kuendeleza mawazo machache yaliyochuguliwa.


KARIBU KATIKA CHANGAMOTO LA USALAMA WA WANAWAKE

Usalama ni msingi wa haki za kibinadamu. Bado mamilioni ya wanawake na wasichana kote duniani wanaishi katika mapato ya chini. Kwao, shida za usalama wa kibinafsi  inatokana na unyanyasaji wa kijinsia, kijamii, kutengwa au ukosefu wa huduma muhimu za kijamii.
 
Pamoja katika changamoto hili, tunawaomba watu binafsi au mashirika kote duniani wabadilishane mawazo na washirikiane pamoja, ili kusaidia kujenga na kuvumbua suluhisho la kufanya miji iwe na usalama zaidi, ili kuwapa Kipaumbele wanawake na wasichana katika mazingira bora. 


LENGO KATIKA MIJI

Ripoti za UN Habitat ya hivi punde yaonyesha kwamba asilimia 70 ya wanawake in baadhi ya watu maskini katika nchi tofauti. Inajulikana kwamba wanawake na wasichana wanaoishi katika mapato ya chini kwenye mazingara ya miji wanaathiriwa na maovu au matitizo kama vile unyanyasaji wa kijinsia, ukosefu wa nyumba imara, vifaa vya usafi au ukosefu wa umeme. Halaiki ya watu katika nchi zinazoendelea wanahamia katika miji kutoka maeneo ya vijiji ili kutafuta suluhisho la usalama kwa wanawake na wasichana.

 

JINSI YA KUWASILISHA WAZO LAKO

  1. Fungua maelezo yako.Ongeza habari kwa maelezo yako, kama ujuzi , uzoefu, maono na kazi. Jamii itakuona, wewe ni nani na nini maslahi yako ni nini!
  2. Kwenda kwa ukurasa ya changamoto za na bonyeza ongeza wazo lako.
  3. Fuata maelekezo katika fomu ili kuwasilisha wazo lako. Unaweza kupendekeza mradi mpya au jinsi ya kuboresha kazi yako.
  4. Kuanza.
  5. Tafadhali ongeza Tafsiri hapa kwa Kihispania

​MAWAZO WA KUANGAZA

Katika mwanzo wa changamoto hili, tumeshirikiana katika awamu ya Utafiti, kutambua masuala muhimu ya kuzingatia. Hapa kuna mambo sita ya kutoa ufafanuzi na mwelekeo. Tunawakaribisha kutumia haya kuchambua na kujenga mawazo yenu.
 

Kujiepusha na Hatari za kisasa: Mara nyingi, wanawake na wasichana hukosa zana bora au huduma ya kuwasaidia kuepuka hatari,kujikinga na hali fulani au kuripoti ya uhalifu katika wakati unaofaa. Jinsi tunaweza kutengeneza mbinu, habari au taratibu ambao wanawake wanaweza kutumia wakati wanajipata katika hatari?


Kuboresha nafasi bora katika miji kupitia mipango ya jamii: Baadhi ya maeneo na hali kama mabasi, mbuga za wanyama, nyika, barabara, kikundi cha watu au uwiano mbaya wa kijinsia huwa inatishia juhudi za wanawake na wasichana. Mabadiliko ya mazingira katika miji yana madhara makubwa. Jinsi tunaweza kufanya mabadiliko kutumia watu binafsi au mashirika ili tufanye usafiri katika miji izingatie jamii?


Kuimarisha Wanawake Kiuchumi: Usalama izingatie tishio la madhara ya kimwili pekee, hila maarifa, ujuzi, mafunzo na uhuru wa kifedha ili  tujiamni katika hali yoyote. Jinsi wanawake na wasichana katika maeneo ya mijini wawaze kujiamini na kujiwezelesha kiuchumi?

 

Changamoto za kijinsia na viashiria: kuimarisha mazingira bora ya wanawake na wasichana katika maeneo ya miji ili wazungumuzie tabia zao za kijamii, matarajio na vikwazo vya kitamaduni. Mara nyingi wao uzuiwa kuzungumza juu ya haki zao na kufurahia faida ya miji wanaoishi. Jinsi  tunaweza kushirikisha wazazi, walimu, wanaume na wavulana kujenga mazingira bora ya wanawake na wasichana?


Ushawishi na usaidizi wa Vikundi: Vikundi vya wanawake ulimwenguni kwote na hata nyumbani zinaweza kutoa nafasi kwa wanawake kusema mambo yao kwa huru, kubadilishana mawazo na rasilimali. Katika hakati ya kutumia teknolojia ulimwenguni kwote, ni bora kuunganisha wanawake kutoka sehemu tofauti, ili waweze kubadilishana taarifa muhimu na hadithi. Jinsi tunaweza kuimarisha uhusiano kati ya wanawake ulimwenguni kwote and hata hapa nyumbani?


Kuendesha fikira kupitia Ushirkiano:  Watu binafsi na mashirika wanaweza kuathiri mabadiliko kupitia sera na utawala. Jinsi tunaweza kusimamia mabadiliko katika mashirika kama vile sera mpya, utekelezaji au utoaji wa huduma bora ili ilete ushirikiano katika jamii?